CHIEF NTINGINYA SECONDARY SCHOOL

CHIEF NTINGINYA SECONDARY SCHOOL
mkuu wa shule akiwaapisha viongozi wa wanafunzi baada ya uchaguzi

Thursday 28 April 2016

CHIEF YAJICHIMBIA KILELENI BASHE CUP

Timu ya sekondari ya chief ntinginya inaongoza kundi B zikiwemo timu za shule za sekondari za badri, Nzega day na itilo baada ya kuzichakaza vizuri timu ya badri na nzega day na hivyo kujijengea mazingara mazuri ya kuongoza kundilo lao, mechi ya mwisho inayosubiliwa kwa hamu ni kati ya chief vs itilo, ilifanikiwa kushinda basi itakutana na mshindi wa pili kutoka kundi A lililo na timu za uchama, samora, ijanija na FDC. 

Saturday 15 August 2015

Mitaala ya Elimu Tanzania

Mitaala ya Elimu katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu imewekwa katika tovuti hii.
Mitaala hii ni ile iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2005 ambayo ilizingatia ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana badala ya ule wa awali unaozingatia maarifa. Mitaala hii imekuwa ikitumika kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2005 hadi hivi sasa.
Mitaala imeboreshwa kufuatia mchakato wa majadiliano katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyofanyika mwezi Februari 2013, pamoja na maoni na hoja mbalimbali zilizotoka kwa wadau wa elimu.
Pamoja na maboresho yaliyofanyika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweka mitaala hii wazi kwa wadau wote wa elimu na jamii kwa ujumla ili kuendelea kupata maoni zaidi ya jinsi na namna ya kuiboresha mitaala hiyo.
Aidha, katika kipindi hiki cha kukusanya maoni, mitaala hii itaendelea kutumika hadi hapo mchakato wa kuihuisha utakapokuwa umekamilika. BOFYA HAPA KWA MAELEZO ZAIDI